TANZANIA

Dk. Tax Aapishwa Kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT Tanzania

SEPTEMBA 1, 2023
Border
news image

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha rasmi Dkt. Stergomena Lawrence Tax baada ya kumhamisha kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kwenda Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania kuwa Waziri mwenye dhamana ya Wizara hii uliofanyika tarehe 01 Septemba, 2023 Ikulu ndogo ya Tungu, Zanzibar.

Uhamisho huo unafuatia mabadiliko madogo aliyoyafanya katika Baraza la Mawaziri na

Waziri Stergomena anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Wizara mpya ya Ujenzi.

Hii ni mara ya pili kwa Dkt. Stergomena kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuiongoza Wizara ya Ulinzi na JKT kwani mara ya kwanza Mheshimiwa Tax aliteuliwa na Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu kuwa Wziri wa Ulinzi na JKT tarehe 12 Septemba, 2021 nafasi aliyohudumu hadi tarehe 02 Oktoba, 2022 alipohamishwa kwenda kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki hadi anahamishwa tena kurudi Wizara ya Ulinzi na JKT.

Uhamisho wa Mawaziri hawa unafuatia Mabadiliko Madogo ya Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu uliofanywa na Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu katika mabadiliko yaliyotangazwa tarehe 30 Agosti, 2023 Rais ameanzisha nafasi ya Naibu Waziri Mkuu anayeshughulikia shughuli za Serikali na kuifuta Wizara yaUjenzi na Uchukuzi na kuunda Wizara mpya mbili ambazo ni Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi na kuteua mawaziri wawili wapya watakaoziongoza Wizara hizo.

Mawaziri wapya walioteuliwa kuongoza Wizara hizo ni Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa atakayekuwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Mheshimiwa Prof. Makame Mnyaa mbarawa atakayekuwa na dhamana ya kuiongoza Wizara ya Uchukuzi.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania