TANZANIA

DART Tanzania Kuanza Kutumia Teknolojia ya Smart Card

AGOSTI 28, 2023
Border
news image

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imetoa ushauri kwa uongozi wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART) kuanza kutumia tekinolojia ya Smart Card ili kuweza kupunguza kero inayoweza kutokea katika upatikanaji wa tiketi kwa abiria na kudhibiti mapato.

Pia kamati imewataka DART kuweza kuongeza idadi ya mabasi ambayo yataweza kupita kwenye miundombinu ambayo wanaiandaa sasa.

Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya TAMISEMI Mhe. Justin Nyamoga Wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI ilipokagua miradi inayotekelezwa na DART katika Mkoa wa Dar Es Salaam.

“Ili kuepuka ulipaji fidia wa mara kwa mara wakati wakuongeza miundombinu tunaihitaji kuhifadhi eneo kubwa la kutosha hasa katika miji inayokuwa ili kuwa na maeneo kwaajili ya uendelezaji wa miundombinu hapo badae” amesema Mhe. Nyamoga

Aidha Makamu Mwenyekiti amewataka katika sehemu yenye makazi ya watu wengi kuwe na umwagiliaji wa maji wa mara kwa mara ili kupunguza kero na maradhi kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo hasa katika kipindi hiki cha ujenzi.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania