TANZANIA

Bodi Ya Wakurugenzi Ya Tawa Yafanya Ukaguzi Wa Kikosi Maalumu Cha Mbwa Jnia

SEPTEMBA 18, 2023
Border
news image

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko imefanya ziara ya Ukaguzi wa kikosi cha Mbwa katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kujionea shughuli zinazofanywa na kikosi hicho katika eneo hilo, kuhakiki ufanisi wake na kuboresha utendaji

Akizungumza na Maafisa wa Uhifadhi na Askari wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam na Pwani pamoja na kikosi cha K9 kinachojumuisha Askari Wenye mafunzo maalumu kwa ajili ya ukaguzi wa nyara za maliasili katika viwanja vya ndege na bandariJijini Dar es Salaam, Mej. Jen. (Mstaafu) Semfuko amewasisitiza wahifadhi hao kuwa na mahusiano mazuri katika shughuli zao Ili kuzilinda rasilimali za nchi.

"Ninyi ndio waanzilishi na ndio mtakuwa viongozi wakuu hapo baadae wa Unit hii hivyo TAWA tunatakiwa kuwa wabunifu wa viwango vya juu” amesema

Nae Naibu kamishna wa Uhifadhi TAWA, Mlage Kabange amesema wameridhishwa na kazi nzuri ya udhibiti na ukaguzi wa nyara zinazotoka na kuingia hapa nchini, kwahiyo katika eneo la uwanja wa ndege jukumu hili linafanyika vizuri kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za ulinzi na Usalama katika kudhibiti wa utoroshaji wa nyara nje ya nchi.

"Mabadiliko haya chanya hayajaja kwa bahati mbaya, kunasababu ambazo zimefanya tuwe na mabadiliko makubwa na chanya kama haya ni Uadilifu, Uwajibikaji, Nidhamu ya hali ya juu, Mikakati na timu work" tunategemea juhudi zaidi na weledi zaidi katika kutekeleza majukumu yenu, alisema mmoja wa wajumbe wa bodi Prof. Jafari Kideghesho.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja Cha Ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere, Lugano Mwansasu ameeleza mafanikio yanayopatikana katika udhibiti wa nyara za serikali viwanjani hapo kupitia TAWA.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania