TANZANIA

BMH Tanzania Kuhudumia Zaidi ya Wananchi 500 wa Mkoa wa Katavi

SEPTEMBA 12, 2023
Border
news image

Madaktari Bingwa na wataalamu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya Jijini Dodoma nchini Tanzania wameanza kambi rasmi ya matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, mkoani Katavi.

Dkt. Alphonce Chandika, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa amesema wameamua kuutembelea mkoa wa Katavi kwakuwa wamekuwa wakipokea wagonjwa kutoka mkoa huo.

"Lengo letu ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ilipoagiza kuwafikia wananchi wasio na uwezo na kuwapa huduma za kibingwa, tupo hapa leo kuwa hudumia wanakatavi tumejipangia malengo ya chini ni kuwahudumia wananchi wasiopungua 500 katika magonjwa mbalimbali yanayo hitaji matibabu ya ubingwa" alisema Dkt. Chandika

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji na watumishi wa BMH kwa kuamua kuwapa kipaumbele wananchi wa Katavi.

"Hospitali ya Benjamin Mkapa imekuwa kimbilio la watu wengi nchini na hata wakazi wa Katavi wanakimbilia Benjamin Mkapa ni kwasababu ya huduma mnazo zitoa zipo katika viwango vizuri na vinavyo jenga imani kwa mgonjwa" alisema Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Hospitali ya Benjamin Mkapa imekuwa ikiwafikia wananchi katika mikoa mbalimbali katika Huduma zake za huduma MKoba (Out reach Services) Jumla ya Madaktari Bingwa 11 wamefika mkoani Katavi ambapo watatoa huduma mbalimbali kuanzia leo mpaka ijumaa ya Tarehe 11/09/2023.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania