TANZANIA

Bilioni 6.7 Zaboresha Huduma Za Afya Handeni – Tanga

OKTOBA 02, 2023
Border
news image

Naibu Waziri wa Afya nchini Tanzania Dkt. Godwin Mollel amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili ameleta kiasi cha shilingi billion 6.7 kwenye Halmashauri ya wilaya ya Handeni ikiwa ni kwa ajili ya Uboreshaji wa Huduma kwenye sekta ya Afya Nchini.

Dkt. Mollel amebainisha hayo wakati akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga nchini Tanzania.

Dkt. Mollel amesema kuwa amepokea maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ni ya kuangalia kwa karibu kwani iko karibu na barabara ya njia panda chalinze kwenda Tanga ambapo kunatokea ajali nyingi hivyo lazima iwe na mahitaji yote muhimu kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya dharura yatakayo tokea wakati wowote.

Aidha ameeleza kuwa mpaka sasa katika hospitali hiyo Huduma zinazopatikana ni Huduma za wagonjwa wa nje, Huduma ya X RAY, Huduma za maabara na Huduma za upasuaji.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania