TANZANIA

AWESO AFANYA MABADILIKO YA WATENDAJI MAJI RUFIJI KWA KUMUONDOA KWENYE NAFASI YAKE MKURUGENZI UTETE

JANUARI 29, 2024
Border
news image

Waziri wa Maji nchini Tanzania Mhe Jumaa Aweso amefanya mabadiliko ya kiuongozi katika Mamlaka ya maji Utete kwa kumuondoa kwenye nafasi yake Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo bwana Christopher Mwigune akiwa wilayani Rufiji alipofanya kikao maalum cha kuongea na Watumishi wa Sekta ya Maji wilaya ya Rufiji na wilaya jirani za mkoa wa Pwani.

Awali Waziri Aweso alifanya mabadiliko ya kiutendaji eneo la Maji Vijijini (RUWASA) kwa mabadiliko ya Meneja wa Wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine,Waziri Aweso amemtambulisha rasmi kwa uongozi wa serikali ya Mkoa na Wilaya Meneja mpya wa wilaya wa Maji Vijijini (RUWASA) Eng Alkam Omari Sabuni na kumuelekeza pia Kukamimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Utete katika kipindi hiki cha Mpito ambacho ataifanya mabadiliko makubwa mamlaka hiyo na kuiunda upya.

MTV Tanzania