TANZANIA

WEKEZA KATIKA UTAFITI KUCHOCHEA MAENDELEO: DKT. BITEKO

MEI 14, 2024
Border
news image

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati nchini Tanzania Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu na mchango wa utafiti wa kisayansi katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisayansi zinazochangia kuchochea maendeleo ya nchi.

Dkt. Biteko ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango katika ufunguzi wa Mkutano wa 32 wa Masuala ya Utafiti wa Kisayansi ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

MTV Tanzania