ITURI

Watu Zaidi ya kumi wauwawa katika Kijiji cha ndimo wilayuani Irumu mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa Congo DRC.

MEI 14, 2024
Border
news image

Shirika la raia eneo hilo kupitia mmoja wao Christophe munyanderu wakishutumu wapiganaji wa ADF kuhusika na mauaji ambayo yalitokea kwa saa za usiku wa leo ,wanawake na Watoto wakiwawa kwa shoka na mapanga.mauaji haya yana jiri wakati serikali mkoani yajipanga kumpokea Rais wa congo Felix Tshiskedi .

Rais wa Congo Felix TSHISKEDI wa Congo alisema kwa sasa amani inatarajia kurudi mkoani Ituri baada ya makundi yenyi kushikilia silaha kukubali kuungana na kuunga mkono juhudi za serikali za kutafuta amani na usalama kwa wananchi wa iTURI.Makundi yenye silaha mkoani Ituri ilikubaliana siku zilizo pita kuacha mapigana kati yao na kupisha mchakato wa umoja.

Mkoa wa Ituri umekuwa ukishuhudia machafuko kwa muda mrefu ,vijiji na kambi za wakimbizi wa ndani zikishambuliwa mara kwa mara na wapiganaji wenye silaha ambao wote kwa jumla wamekubali kuweka silaha chini na kujenga umoja kwa ajili ya maendeleo ya mkoa ambao una madini mengi.

AM/MTV DRC ONLINE