DRC SADC

Wanajeshi wanne kutoka Ujumbe wa SADC katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (SAMIDRC) wamefariki Dunia mashariki mwa DRC .wakiwemo tatu kutoka Tanzania na mmoja kutoka Africa kusini .

Aprili 09, 2024
Border
news image

Katika tangazo la SADC nikwamba wanajeshi hao walifariki Dunia baada ya kushambuliwa na mbomu kutoka upande wa waasi wa M23 kwenye milima inayo zunguuka mji wa Sake unao patikana kilometa ishirini magharibi mwa Mji wa Goma Kivu Kaskazini.

SADC inasema wanajeshi hao wamefariki Dunia wakiwa katika mchakato wakutafuta amani mashariki mwa Congo.ambako serikali ya Congo DRC inapambana na waasi wa M23 .wanajeshi kutoka Africa kusini ,Tanzania na Malawi wako Goma na Masisi kushirikiana na jeshi la Congo kuulinda Mji wa Goma ili usitekwe na waasi wa M23.

Masharika ya kiraia imeomba SADC kuingia moja kwa moja katika mapigano kuwatimua waasi wa M23 kwenye milima ya Mji wa Sake kwani sasa waasi hao ni tishio kwa taifa la DRC ba kwa wakimbizi wanao patikana katika kambi mbali.

Alipokuwa Mjini Kigali juma Pili Rais wa Africa Kusini alisema mzozo wa mashariki mwa Congo lazima kutatuliwa kidiplomasia kuepuka matokeo mabaya ya mauaji.

M23 kwa upande wake ikisema njia bora ya kumaliza vita mashariki mwa Congo ni Mazungumuzo ya kisiasa kuliko kutumia nguvu yaani silaha.

AM/MTV DRC ONLINE