Pharmakina inashika nafasi ya kwanza ili kukidhi matarajio ya Mpango Mkuu wa Uendelezaji wa Viwanda (PDI) katika secta ya tibabu nchini Jamhuri ya Kidemocratia ya Kongo (DRC), Kupitia utaalamu wake katika kubadilisha asilimiya mia moja ya gome la cinchona hadi kuishia dawa ya kwinini (Quinine) ,kwinine ambayo yatumika sana katika kutibu ugonjwa malaria ambao waua maelfu ya watu barani Africa hasa Congo DRC.. Kampuni hii inataka kuongeza uzalishaji wake ili kupambana na malaria.
Alhamisi hii, Septemba 7, ujumbe ulio kuwa na Kiongozi wa kampuni hii, Afisa Mkuu Mtendaji wake (CEO) na Msimamizi wake walikutana na Waziri wa Viwanda wa Kongo Mjini Kinshasa. Kwa pamoja, walitafakari jinsi serikali inaweza kusaidia Pharmakina kuongeza uzalishaji wake na wa wakulima wa cinchona.
Kwa sasa Mlimo wa Quenquina umedidimia pale Pharmakina ilianza kupunguza shughili zake mashariki mwa Congo hasa Kivu Kaskazini na Kivu Kusini ambako kulionekana uzalisha mkubwa kwa muda mrefu wa mimea hiyo ya Quinquina.
“Tulikuja kuonana na Waziri ili kumweleza shughuli zetu, sisi ndiyo kampuni inayobadilisha kwinini kuwa dawa dhidi ya malaria. Tunadhani tuna uwezo mkubwa wa kuendeleza sekta hii. Kivu ni chanzo cha miaka 8 cha asilimiya mia moja ya rasilimali za ulimwengu za cichina. Kiwanda chetu ndicho pekee barani Afrika ambacho kinachakata magome ya cinchona ya kipekee sana ambayo huokoa mamilioni ya maisha,” alieleza Roland Decorvet, Kiongozi wa Pharmakina.
Kampuni ya Pharmakina kwa hivyo inataka kuwa kitovu cha umahiri katika utengenezaji wa kwinini; na kutaka kuungwa mkono na serikali kupitia Wizara ya Viwanda ya Kongo.
“Tunataka kukipanua kiwanda hiki, tunataka kiwe kitovu cha umahiri ili kweli kuweza kusambaza bidhaa nyingi zaidi, madawa, iwe Kongo au nchi jirani. Ni kweli, tunahitaji msaada, msaada kutoka serikalini,” alieleza.
Roland Decorvet alisifu ujuzi wa Waziri wa Viwanda wa Kongo, Julien Paluku wa sekta ya uzalishaji wa matibabu. Anasema amefurahishwa na nia hii ya Wizara ya Viwanda ya Kongo kutoa nishati zaidi kwa bidhaa asilia, ili kuinua kiwango cha wazalishaji wa ndani.
Waziri wa Viwanda na wajumbe wa Pharmakina wamekubaliana kuweka mpango wa kuongeza uwezo wa uzalishaji wa kampuni hii, mpango wa mafunzo na maendeleo kwa wakulima wa cinchona wa Kivu ili kuongeza mavuno yao ambayo moja kwa moja yataongeza uzalishaji wa Pharmakina.