DRC

DRC watu tisa wafariki Dunia na wengine ambao idadi yao haijulikane kutekwa na watu wanao dhaniwa kuwa ADF pa Mantumbi wilayani Beni Kivu Kaskazini.

MEI 09, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV News DRC Jonathan Hangi ni Mkaazi kutoka vijiji vya Mantumbi ambako Watu Zaidi ya nane wameuwawa katika Kijiji chao kinacho katikati mwa Miji ya Mangina na mbau ,Oicha Makumo ambako watu wanao dhaniwa kuwa ADF walivaamia makaazi ya watu kwa saa za usiku na kuwauwa watu kwa shoka ,mapanga na hata kuchoma nyumba na kuwateka wengine ambao idadi kamili haijulikane asema watu wanao dhaniwa kuwa ADF wali vaamia makaazi na kuanza kuwafunga vinywa wakaazi na kuwakata vichwa ,miongoni mwao wanawake na Watoto n ahata watu wazima.

Jonathan Hangi mkaazi wa Mantumbi ansema walijaribu mara kadhaa kuwapigia simu viongozi bila mafanikio swala linalo wakera kwa sasa kuona mauaji kuendelea eneo lao bila kukomesha. Mkaazi huyu ameongeza kwamba mauaji ya Beni nikama ina sababu yake kwani kuna kikosi kikubwa cha MONUSCO ambacho bado kimesha shindwa kuzima mauaji hayo

Miongoni mwa walio uuwawa ni mfanya kazi wa kituo kimoja cha Afia Cha cha Mantumbi SARU ambako watu wengi wametekwa na kubebwa porini akisema Saidi Balikwisha mbunge wa Beni Kutoka vijiji vya ISALE VULAMBO ambae alipata kura nyingi siku zilizo pita asema tataizo kubwa kwa sasa nikwamba bado kuna tatizo kubwa kutokana kwamba miezi tano sasa tangu uchaguzi kukiwa hakuna serikali mpya na wao kama wabunge hushindwa kuelekeza malalamiko ya wakaazi Kinacho onekana nikuwa serikali imeshindwa kuhudumisha usalama wa wananchi wa Beni wanao uwawa tangu mwaka wa elfu mbili na kumi(2010)

Jeshi la Congo FARDC eneo la Beni likiomba ushirikiano wa wananchi na wanajeshi Pamoja na vyombo vyote vya usalama akisema Antony Mwaluchayi msemaji wa operesheni Sokola ya kwanza akiwa Beni Kivu Kaskazini ( wanajeshi wanao pigana,Rai na jeshi wote wapashwa ungana Pamoja kwani husema usalama ni wakila mwananchi hakuna anae kuwa juu ya mwengine)

Nae Kizerbo Kasereka wathevwa mbunge wa zamani wa Beni alie kuwa katika shirika za Kiraia. Akiomba raia kushirikishwa katika msako wa ADF hasa kutumia mtindo wa vijana wazalendo kwani ni vigumu sasa jeshi kuwajibika na kufikia kila Kijiji

Mauaji ya Beni imeanza tangu mwaka wa elfu mbili na kumi katika vijiji Operea na mayimoya Pamoja na kikingi Rwenzori hadi sasa ,maelefu ya watu wakipoteza Maisha na wengine kutekwa katika uangalizi wa serikali,MONUSCO na SADEC kwa sasa UPDF.lakini bado mauaji ikiendelea vijiji vikichomwa na watu kuhama makaazi yao. Umoja wa Matifa kupitia MONUSCO husema kwamba wamekuja DRC kuwalinda raia lakini idadi ya uhali ikiongeza Zaidi tangu pale kikosi hicho kipo nchini Congo DRC ambako kina kemewa na wakaazi kushindwa kutekeleza majukumu yake.

AM/MTV DRC ONLINE