DRC

DRC Wanawake mashariki mwa Congo waomba Rais wa Tanzania kuingilia swala la usalama DRC.

Aprili 22, 2024
Border
news image

Katika kikao cha zarura kilicho fanyika kwenye jingo la wanawake Mjini Goma .makundi mbali mbali ya wanawake mashariki mwa Congo wasema kwa sasa wamechoshwa na hali ya mateso wanayo shuhudia wanawake katika kambi mbali kutokana na uasi usio kuwa na sababu mashariki mwa Congo.

Poline wa Maria mmoja wa wanawake wanaharakati eneo hili asema vita vya Congo sasa Vimedumu muda mrefu n ani swala lisilo eleweka ,kinacho hitajika kwa sasa ni kuwaleezea wakaazi wa Congo DRC sababu kubwa ya vita vinavyo wapelekea kuteseka .kwa sasa wamejipanga kwenda Tanzania kukutana na Rais Samia Hassani Suluhu ambae wanadhani anaweza kusikiliza wanawake wenzie .

Wengi wakisema wamebaki wajane kutokana na mapigano ya mara kwa mara ,bwana zao na Watoto wakiuwawa kwa risasi na uasi unao tokea kilamara nchini Rwanda.Rwanda imekuwa ikisema inatuma majeshi yake eneo la mashariki mwa DRCongo kuwatafuta FDLR lakini wachambuzi upande wa DRC wakiwa na mtazamo tafauti.kwani Rwanda iliwahi kuongoza Taifa la Congo DRC kwa miaka mitano na kuweka makamanda wake kote mashariki mwa Congo katika Mikoa ya Kivu Kaskazini,Kivu Kusini,Ituri,Maniema ,Katanga n ahata Tshopo katika harakati wanao ita kutafuta FDLR .

Serikali ya Congo ikishutumu Rwanda kuwauwa maelefu ya raia wa Congo katika Vita mbali mbali ikiwemo vita vya Makobola Mkoa wa Kivu Kusini na wengine wilayani Rutshuru eneo la Rugari wakati wa uasi mbali mbali .

Wananchi wa Congo wameomba jumhia ya Kimataifa kutafuta suluhisho la haraka kuhusu mzozo wa mashariki mwa Congo kwani mataifa yote imekuwa ikikiuka mikataba ya AU ikiwa hakuna taifa ambalo linaweza vaamia ama kulikia linguine waasi.rwanda ikishutumiwa kuunga mkono waasi wa M23 na kuweka waasi wa Congo nchini Rwanda na Rwanda ikishutumu DRC kuwaweka FDLR nchini DRC.lakini Congo ikisema sababu kubwa ya Rwanda kuvaamia DRC nikupora mali yake na kuvaamia ardhi .

Wakaazi wakisema kumekuwa mikataba nyingi ambayo kwa sasa wakaazi wenyewe hayafahamu.

AM/MTV DRC ONLINE