DRC

DRC wafanya kazi nchini DRC waomba sheria kuhusu wafanya kazi kurekebishwa hasa kuhusu mshahara wao.

MEI 02, 2024
Border
news image

Siku moja baada ya siku ya wafanya kazi Duniani ,wafanya kazi nchini DRCongo wasema mshahara kwa wafanya kazi wa Congo DRC ni mdogo japo waishi katika taifa Tajiri ambalo laomba uongozi bora. Wengi mwao wakisema Dola imekuwa chanzo cha malipo yao kuwa Duni Zaidi na kushindwa kujibu mahitaji ya familia.

Siku ya wafanya kazi nchini DRC imekuwa kilio kwa wengi hasa waalimu na na wafanya kazi wengine katika vyombo vya usalama .mashirika ya kiraia ikiomba bunge kuweka sheria mpya ya kuongeza mshahara kwa wanajeshi na wafanya kazi wengine wa serikali kwa ajili ya usalama na ulinzi wa taifa . Taifa la Congo likipitia hali mbaya na ngumu ya kiusalama mashariki mwa Congo ambako kuna maelfu ya wakazimbizi wa ndani wakiwa bila msaada kambini.

Vijana wanao maliza shule wakiomba kuajiriwa,ajira upande wa Congo ikiwa mitihani mkubwa sana kutokana na hali ya kisiasa ,wana siasa wakiendelea ku ajiri watu wa familia kuliko kuajiri watu wanao stahili .wanafunzi wanao maliza shule wameomba Rais Felix Tshisekedi kujaribu kuwapa ajira vijana ambao wamekuwa mustari wa mbele na wakiwa ndio wengi wanao kuwa bila ajira na kaumua kujiunga na makundi mbali mbali yenye silaha ama uhalifu na wengine kujiunga na shirika za kiraia kama kuweka presha kwa serikali.

AM/MTV DRC ONLINE.