DRC

DRC Serikali ya Congo DRC ya laani vikali mauaji ya raia wa Taifa lake inayo tekelezwa na taifa Jirani la Rwanda asema albert Fabrice Puele Waziri wa kiutu nchini DRC.

MEI 10, 2024
Border
news image

Akizungumuza na vyombo vya Habari baada ya kukutana nae Gavana wa Kivu Kaskazini Meja Generali Perter Cirimwami ,Albert Fabrice Puela Waziri ahusikae na haki za binaadamu nchini Drcongo asema Rwanda lazima kujibu vitendo wanavyo tekeleza nchini DRC kwa muda mrefu hasa mauaji ya raia wa congo .Puela amasema kisa cha hivi karibuni na shambulizi la kambi ya Mugunga Mjini Goma ambako watu thelanithini na tano wamefariki Dunia na wengine thelathini na sita kujeruhiwa.

Puela amesema kwa sasa serikali ya Congo inakusanya matokeo mbali mbali ambayo taifa la Rwanda na wasaidizi wake wa M23 wanatekeleza na siku moja watajibu hata baada ya miaka ishirini.kwa uapnde wake Modeste Mutinga Mutushayi ,kitendo kilicho tekelezwa na Rwanda Pamoja na washirika wake wa M23 haitakubalika na serikali pampoja na raia wa Congo kwani sheria za kibinaadamu haziruhusu kambi ya wakimbizi kushambuliwa na mutu yeyote.

Mutinga ameandamana na timu kubwa la wabunge na wajumbe wengine wa serikali ambao wametangaza kuanza mazishi ya watu walio uwawa wiki ilio pita kwa bomu kutoka upande wa waasi wa M23 ,Mutinga amesisitiza kwamba walio fariki wote watazikwa na serikali ya Congo hii juma mosi Mjini Goma kwa heshima na kuomba jumhia ya kimataifa kuepuka kuegemea upande mmoja katika mzozo wa DRC.

Fabrice Puela kwa uapnde wake ametuhumu umoja wa mataifa kutojali wananchi wa Congo na kuegemea upande mmoja yaani Rwanda ambayo ndio chanjo cha mateso ya raia wa Congo DRC ,nakulazimisha maelfu ya watu kuhama makaazi yao.

Rwanda imekuwa ikikanusha uwepo wake DRC na kusema mzozo wa Mashariki mwa Congo unahitaji mazungumuzo ya raia wa Congo kuliko utumiaji wa silaha ,Pamoja na kutatua shida la wapiganaji wa Rwanda wa FDLR kwani ndio chanjo cha mzozo kati ya DRC na Rwanda .DRC ikisema imegundua kwamba FDLR wanao tafutwa Congo ni madini ya raslimali.

Vita mashariki mwa Congo vimesababisha maafa mengi ,vifo,ukiukwaji wa haki na msigi za binaadamu Pamoja na kupelekea maelfu ya wakaazi kuwa wakimbizi katika taifa lao.wachambuzi wakiomba mzozo huo kutatuliwa kidiplomasia kuliko mapigano.

AM/MTV DRC ONLINE.